Yanga Princess imetakata uwanja wa Uhuru leo baada ya kuifumua Tiger Queens mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake, Serengeti Lite
Blessing Nkor ameendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu kwenye ligi hiyo akifunga hat-trik
Mabao mengine ya Yanga Princess yalifungwa na Wogu pamoja na Nadege
Yanga Princess imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 17 ikiwa sawa na JKT Queens lakini Yanga Princess ikiwa na uwiano mzuri wa mabao
Hata hivyo msimamo huo unaweza kubadilika kutegemea na matokeo ya mechi ambazo zitapigwa kesho



ADVERTISE HERE