Baada ya makundi, tuitafute robo fainali Shirikisho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2023
Baada ya makundi, tuitafute robo fainali Shirikisho

Kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga imepanda katika orodha ya ubora kutoka nafasi ya 75 mpaka nafasi ya 48

Wananchi wanapaswa kupambana kwelikweli angalau kutinga robo fainali ili kujiongezea alama ambazo zitawafanya waendelee kupanda juu kwenye viwango vya CAF

Yanga imekusanya alama 2.5 (0.5x5) kwa kufanikiwa kutinga makundi. Alama hizo zitaongezeka kama watamaliza nafasi ya tatu au kwenda juu

Wakimaliza nafasi ya tatu watakuwa na alama 5 (1x5), wakifanikiwa kutinga robo fainali ni 10 (2x5), nusu fainali ni 15 (3x5), wakitinga fainali ni 20 (5x4) na wakiwa mabingwa ni 25 (5x5)

Kuna faida kubwa kuwa juu kwenye viwango vya ubora vya CAF kwani kwa timu zinazokuwa nafasi za juu kabisa mara nyingi hazishiriki hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa na Shirikisho

Kwa zile timu ambazo ziko juu kwenye viwango lakini hazikufikia sifa ya kutocheza hatua ya awali, mara nyingi hupata ratiba rafiki katika mechi zao kwani hupangwa na timu ambazo ziko chini katika orodha ya ubora

Simba imenufaika na utaratibu huo katika miaka mitano iliyopita baada ya kutinga robo fainali mara kadhaa kwenye ligi ya mabingwa na Shirikisho

Msimu huu Simba hawakuwa na njia ngumu kutinga makundi ya ligi ya mabingwa wakipangwa na Nyasa Big Bullets na De Agosto

Yanga kupangwa na Al Hilal katika raundi ya kwanza ni kutokana na utaratibu huo wa CAF, Yanga ilikuwa nafasi ya 75 kwenye viwango wakati Al Hilal walikuwa katika nafasai 20 bora

Timu inapokuwa juu katika viwango vya CAF inajiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kubaki katika nafasi hiyo kwani angalau kila msimu kuna uhakika wa kutinga hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’