Vyombo vya Habari Zambia vyaripoti Lwandamina kurejea ZESCO

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2018
Vyombo vya Habari Zambia vyaripoti Lwandamina kurejea ZESCO
Wakati Yanga ikiwa mkoani Mtwara leo ikitarajiwa kuivaa Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 19, kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya kocha wake Mkuu George Lwandamina ambaye anatakiwa kwa udi na uvumba na timu yake ya zamani ya ZESCO, mabingwa Zambia.

Lwandamina alijiunga na Yanga mwezi Novemba 2016 akitokea klabu hiyo ya Zambia.

Kwa takribani wiki nzima vyombo vya Habari nchini Zambia vimekuwa vikiripoti kurejea kwa Lwandamina katika klabu ya ZESCO pamoja na msaidizi wake Noel Mwandila.

Kwa sasa ZESCO inanolewa na kocha wa muda Tenant Chembo baada ya kuondoka kwa kocha wake Mkuu.

Habari za ndani kutoka uongozi wa ZESCO zimeeleza kumalizana na kocha huyo aliyeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita.

Hata hivyo mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo kama ZESCO wanamtaka sasa watalazimika kuilipa Yanga fedha za kuvunja mkataba wake.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema uamuzi wa kuondoka au kubaki Yanga ni wa kocha mwenyewe lakini anachofahamu kwa sasa yeye bado ni mwajiliwa wa Yanga kwa kuwa mkataba wake bado haujamalizika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’