Kesho Jumamosi, Februari 04 Wananchi wana jambo lao uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ni msako wa alama tatu kwenye mchezo dhidi ya Namungo Fc, matokeo ambayo yatazidi kuwasogeza Wananchi karibu na ubingwa wa 29
Baada ya mchezo huo Yanga itahamia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF ambapo wanakabiliwa na mechi mbili zitazofuatana
Februari 12 watakuwa ugenini kule Tunisia kumenyana na US Monastir kisha kurejea jijini Dar es salaam kuikabili TP Mazembe kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 19
Iko hivi; Yanga itasafiri kuelekea Tunisia kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya US Monastir
Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya siku tano huko Tunisia kabla ya kuwavaa Monastir Februari 12
Ni mbinu ileile iliyotumika wakati wa mchezo dhidi ya Club Africain, inakwenda kutumika tena
Katika muda huo wachezaji watapata nafasi ya kuzoea hali ya hewa na watakuwa tayari kuwakabili wenyeji wao katika mchezo ambao Yanga inapiga hesabu ya kuvuna angalau alama moja