Mshambuliaji Kennedy Musonda ameanza vyema majukumu yake katika kikosi cha Yanga licha ya kuwa bado hajafanikiwa kufunga
Musonda alitumika kwa takribani dakika 27 kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc na pia kupewa dakika 60 kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Mashabiki wa Yanga wanapaswa kuendelea kuwa na subira, wasikubali kuingia katika mijadala ambayo inaanzishwa makusudi ili kuwaaminisha kuwa mshambuliaji huyo si lolote
Musonda aliondoka Power Dynamos akiwa kinara wa kupachika mabao kwenye ligi kuu ya Zambia akifunga mabao 11
Ni suala la muda tu, ndani ya ligi ya NBC atawanyamazisha wale walioanza maneno maneno
Ilikuwa hivyo hata kwa mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa, sasa hawasikiki tena baada ya Lomalisa kuuwasha moto
Ujio wa Musonda ni ahueni kubwa kwa Mayele ambaye hakuwa na ushindani katika nafasi yake
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anatamani kuwatumia wote wawili pamoja na alijaribu katika mechi mbili zilizopita