Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamekuwa na muda mzuri wa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kaze amesema wanakwenda kuikabili Ruvu Shooting kwa tahadhari kubwa wakifahamu ni timu inayowapa ushindani kila wanapokutana nayo
"Kitu cha kwanza tumekuwa na wiki nzuri tumepata siku saba (7) za kupumzika, siku hizo zimetupatia muda wa kuongeza fitness ya wachezaji sasa ninaweza kusema ilikuwa ni wiki nzuri ya kupumzika na kurekebisha mambo mengi katika timu"
"Mechi yetu na Ruvu haijawahi kuwa nyepesi kabisa, kama inakumbukwa kule Kigoma tulisuluhu. Pointi tatu (3) za kesho ni muhimu sana katika kukusanya zile za kuelekea ubingwa," alisema Kaze
Kaze amebainisha kuwa kiungo Khalid Aucho anaendelea vizuri, baada ya mazoezi ya mwisho leo watafanya tathmini kuona ni wachezaji gani watatumika katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Kuhusu beki mpya Mamadou Doumbia, Kaze amesema beki huyo anaweza kuwakabili Ruvu Shooting kwani vibali vyake vyote vimepatikana
"Inawezekana kesho mkamuona Mamadou Doumbia, lolote linawezekana vibali vyake pia vimekamilika kilichobakia ni kuangalia fitness yake tu kama atakuwa tayari kucheza"