Kiungo wa Yanga Khalid Aucho anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki moja baada ya kuumia mazoezini
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Yanga, Aucho alipata uvimbe kwenye mshipa wa mguu baada ya kuumia katika mazoezi yanayoendelea Avic Town
Aucho alikosa mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc na huenda akakosa mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Jumatatu, Januari 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga inaendelea kujifua Avic Town kujiandaa na mchezo huo ambapo wachezaji wanafanya program mbili za mazoezi, asubuhi na jioni
ADVERTISE HERE