Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema uongozi wa klabu chini ya Mtendaji Mkuu Andre Mtine una utaratibu wa kushughulikia mashuala yanayohusu wachezaji na wafanyakazi wa Yanga
Kufuatia baadhi ya wachezaji kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kurudi kutoka kwenye mapumziko, mashabiki na Wanachama Yanga wameonyeshwa kutofurahishwa na tukio hilo
Kamwe amebainisha kuwa mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu Bernard Morrison ambaye bado hajarejea na suala lake liko chini ya Mtendaji Mkuu
"Sina maelezo kuhusu Morrison suala lake liko chini ya Mtendaji Mkuu, hivyo nasubiri taarifa kutoka kwa Mtendaji juu ya hatua gani zitachukuliwa dhidi yake baada ya kuchelewa kurudi," alisema Kamwe
Morrison aliondoka nchini baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc uliopigwa Disemba 23 akiombe ruhusa kurejea kwao Ghana kushughulikia matatizo ya kifamilia
Alikosa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na jana amekosa mchezo dhidi ya Ihefu Fc