Mechi za raundi ya 20 ligi kuu ya NBC zinatarajiwa kupigwa kuanzia mwishoni mwa wiki hii baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi inayofikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Singida BS dhidi ya Mlandege
Mabingwa watetezi Yanga wao watashuka uwanjani siku ya Jumatatu, Januari 16 kuwakabili Ihefu Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ilifunga mwaka 2022 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 50 kutoka mechi 19
Wananchi wameweka rekodi ya pekee wakiwa timu iliyofunga bao katika kila mchezo
Yaani mashabiki wa Yanga wameshangilia goli katika kila mechi ambayo timu yao imecheza kwenye ligi msimu huu
Fiston Mayele ndiye kinara wa kuzifumania nyavu akiwa amepachika mabao 14 akiongoza kwa tofauti ya mabao manne dhidi ya Moses Phiri wa Simba aliyefunga mabao 10