Yanga kambini kuiwinda Ihefu Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jan 2023
Yanga kambini kuiwinda Ihefu Fc

Kikosi cha Yanga leo kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa Jumatatu, Januari 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya mapumziko ya mwanzo wa mwaka, wachezaji ambao hawakushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi wameingia kambini leo huku wenzao walioshiriki michuano hiyo wakitarajiwa kuingia kesho Ijumaa

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema mechi dhidi ya Ihefu Fc ina umuhimu wa kipekee kwao wakihitaji kushinda katika mkakati wa kutetea ubingwa

Mechi dhidi ya Ihefu Fc ni moja ya mechi ambazo Yanga wanatarajiwa kucheza mfululizo katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kama hakutakuwa na mabadiliko kwa mechi dhidi ya KMC, Yanga itacheza mechi saba mfululizo katika uwanja wa Benjamin Mkapa na pengine inaweza kujihakikishia kutetea ubingwa mapema kama watashinda mechi hizo

Baada ya Ihefu Fc, mechi itakayofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting ambayo itapigwa Januari 21 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Februari 04 katika uwanja huo

Ratiba inaonyesha KMC dhidi ya Yanga nao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa February 22 na kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold ambapo utapigwa March 12 katika dimba la Mkapa

Mtanange wa Simba dhidi ya Yanga utapigwa April 09 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa April 16 katika dimba la Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’