FT : Majimaji 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2018
FT : Majimaji 1-2 Yanga
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamefuzu robo fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuilaza Majimaji mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Jumapili jioni kwenye dimba la Majimaji.

Mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Pius Buswita kwenye dakika ya 40 akiunganisha krosi ya Haji Mwinyi na Emanuel Martin aliyeunganisha krosi ya Hassani Kessy katika dakika ya 57.

Bao la kufutia machozi la Majimaji lilifungwa na Jaffar Mohammed kwenye dakika ya 61.

Mchezo huo haukuwa na ufundi mwingi kutoka upande wa Yanga, hali mbaya ya uwanja ikiwa sababu kubwa kwa Yanga kutotoa burudani ya kutosha kwa Wananchi.

Hata hivyo benchi la ufundi lilifanya 'homework' yao vizuri kwa kuingia na mbinu ya mipira mirefu na krosi ambazo zilizaa mabao yote mawili.

Yanga imeungana na Mtibwa Sugar kufuzu robo fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda katika michezo iliyopigwa leo.

Mtibwa Sugar imeilaza Buseresere mabao 3-0.

Timu nyingine ambazo tayari zimefuzu robo fainali ya michuano hiyo ni Njombe Mji, Singida United na Azam FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’