Kinara wa mabao ligi kuu ya Zambia Kennedy Musonda anahusishwa kujiunga na Yanga, mabingwa wa Tanzania
Musonda anayeitumikia Power Dynamos, msimu huu amefunga mabao 11 katika mechi 18 akiiweka Dynamos kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Zambia
Imeelezwa jina la Musonda liliwasilishwa mezani kwa Kocha Nasreddine Nabi ili kujiridhisha nae kabla ya Yanga kukamilisha usajili wake
Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amehusika kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha nyota huyo anatua Jangwani
Awali Power Dynamos waliweka ngumu kumruhusu aondoke hasa ikizingatiwa ni mchezaji muhimu katika kikosi chao kinachowania ubingwa wa Zambia msimu huu
Vyanzo mbalimbali vya habari vimebainisha kuwa Yanga wamefanikiwa kununua mkataba wake wa miezi sita uliokuwa umebaki na tayari nyota huyo ametua Tanzania kukamilisha usajli wake
Musonda utakuwa usajili wa pili kwa Yanga katika dirisha hili baada ya Mudathir Yahya