Jana mshambuliaji wa Singida BS Mcongoman Fancy Kazadi Kasengu aliiadhibu Azam Fc akifunga mabao manne katika mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi
Kazadi pia alifunga bao kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mshambuliaji huyo ndio kinara wa kuzifumania nyavu katika michuano hiyo akiwa amefunga mabao matano
Kabla ya kutua Singida BS, kwa nyakati tofauti, Kazadi alikuwa akihusishwa na Yanga
Ni wazi baada ya kumshuhudia kwenye michuano hiyo akifanya vizuri, mabosi wa Yanga wanaweza kuinua simu kumpigia Mh Mwigulu Nchemba!
Yanga inasaka mbadala wa Heritier Makambo ambaye ni wazi yuko kwenye wakati mgumu kuendelea kubaki katika kikosi cha Yanga
ADVERTISE HERE