Mabao ya Maimuna Hamis, Amina Bilali, Wincate Kinyua na Aniella Uwimana aliyefunga mabao mawili, yametosha kuihakikishia Yanga Princess ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Alliance Girls
Ni katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake uliopigwa uwanja wa Uhuru, Dar es salaam
Ushindi huo unaifanya Yanga Princess ifikishe alama saba na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite'
Kikosi cha Kocha Sebastian Nkoma kimeanza kuonyesha mabadiliko makubwa ya uchezaji, ni wazi msimu huu wako tayari kuwania ubingwa wa ligi hiyo ya Wanawake
ADVERTISE HERE