Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2022
Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika mkutano na wanahabari leo, Kaze amesema wamejiandaa kukabiliana na Azam Fc katika mchezo ambao utakuwa mgumu

"Tunafahamu Azam Fc wana timu nzuri, wachezaji wetu wanajua umuhimu wa mchezo huu, tunahitaji kushinda ili tuongeze wigo wa pointi dhidi yao"

"Tunacheza na timu ambayo tunashindana nayo katika ubingwa, kwetu ni wakati mzuri wa kuwatoa njiani na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi," alisema Kaze

Akizungumzia utayari wa wachezaji, Kaze amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo akiwemo kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'

"Tumefanya mazoezi kwa siku mbili, wachezaji watakaotumika kesho ni wale ambao wako tayari na wamefanya mazoezi vizuri. Feisal anaweza akatumika kwa sababu amefanya mazoezi kwenye siku hizi mbili za nyuma na tunaamini ni mchezaji ambaye anaweza kukupa kitu tofauti uwanjani"

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’