Jezi nyeusi zimewachanganya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Dec 2022
Jezi nyeusi zimewachanganya Azam Fc

Azam Fc nao wameingia kwenye siasa ya jezi nyeusi baada ya aliyekuwa Afisa wao wa Habari Thabit Zacharia kusema kwenye mchezo dhidi ya Yanga watavaa jezi nyeusi ili kumuenzi Mdhamini wao

Azam Fc watakuwa mwenyeji wa Yanga siku ya Jumapili katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 2 usiku

Ni wazi kasi ya Yanga imewatia kiwewe hasa wanapovaa jezi nyeusi! Lakini huo ni utaratibu ambao Yanga wenyewe waliutengeneza na kuamini kuwa wakivaa jezi nyeusi hawapotezi mchezo

Lakini ukweli ni kuwa jezi  nyeusi, njano na hata kijani zote ni sawa, walichotengeneza Yanga ni 'mind game' ambayo tayari imewaathiri wapinzani wake

Kuna wakati Afisa Habari wa Bodi ya Ligi alidai Yanga wanaweza kuadhibiwa kwa kuvaa jezi nyeusi katika kila mchezo pasipo kujua zipo kanuni ambazo zinasimamia utaratibu wa mavazi kwenye mechi

Yanga wanaweza kuvaa jezi yoyote miongoni mwa jezi zao walizozitambulisha katika msimu husika ili mradi tu haifanani na jezi ya mpinzani

Jumapili kama Azam Fc watavaa jezi nyeusi basi Wananchi watarudi kwenye uzi wao wa njano au kijani na soka litapigwa kama kawaida

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’