Dalili za ubingwa wa 29 zimeanza kuonekana mapema tu baada ya Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC huku washindani wake Simba na Azam Fc wakiendelea kudondosha alama
Jana Azam Fc walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Geita Gold matokeo ambayo Simba pia waliyapata dhidi ya Kagera Sugar
Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya alama sita ikiwa na alama 44 wakati Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 38
Azam Fc wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 37 huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 17
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili, Disemba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Alama tatu kwa Yanga zitawaweka Wananchi katika nafasi nzuri zaidi kwenye mbio za ubingwa

ADVERTISE HERE