Tutaongeza wachezaji wawili dirisha dogo - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2022
Tutaongeza wachezaji wawili dirisha dogo - Hersi

Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema wamejipanga kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha dogo la usajili kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi

AKizungumza katika Mkutano na Wanahabri mapema leo, Injinia Hersi amesema huu ni msimu wa kuweka alama kwenye michuano ya Kimataifa hivyo wataleta wachezaji ambao wana uwezo wa juu zaidi ya hawa waliopo

"Tumefanya kazi kwa ukaribu na benchi la ufundi na wametupa mapendekezo ya maboresho ambayo wanayahitaji kwa ajili ya kutimiza malengo yetu ambayo ni kutetea makombe yetu pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Shirikisho CAF"

"Tutafanya usajili wa mchezaji mmoja au wawili kwa kuzingatia mapendekezo hayo. Pia tunao wachezaji wawili wa kigeni Yacouba Songne na Lazarus Kambole ambao hatukuwasajili kwenye dirisha lililopita. Wamefanya juhudi kubwa na sasa wako tayari hivyo tumewaachia benchi la ufundi waamue kama watamsajili mmoja au wote wawili"

"Lakini pia kumbuka kama watawahitaji wote wawili ina maana tunahitaji kuondoa wachezaji wawili kwani tayari tuna wachezaji 12 wa kigeni. Mazingira haya yameleta ushindani miongoni mwa wachezaji kila mmoja akitaka kufanya vizuri kila anapopewa nafasi," alisema Hersi

Aidha Injinia Hersi amesema wamepokea maombi kutoka kwa klabu mbalimbali zinazowahitaji baadhi ya wachezaji kwa mkopo

Amesema Yanga ina wachezaji wengi vijana wenye vipaji hivyo wapo baadhi ya wachezaji watawatoa kwa mkopo ili wakapate nafasi zaidi ya kucheza ili kuendelea kuwaimarisha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’