Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi ligi kuu ya Wanawake msimu huu kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess utapigwa siku ya Alhamisi, Disemba 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huo unaozikutanisha timu zenye upinzani wa asili, utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza hakutakuwa na kiingilio kushuhudia mchezo huo
Yanga Princess inayonolewa na kocha Sebastian Nkoma amepania kushinda mchezo huo kikosi kikiweka kambi Avic Town kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo

ADVERTISE HERE