Yanga uso kwa uso dhidi ya Coastal Union leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2022
Yanga uso kwa uso dhidi ya Coastal Union leo

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo vinara wa ligi hiyo Yanga watakuwa wenyeji wa Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 12:15 jioni

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania, Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na dhamira ya kuendeleza pale walipoishia

Alama tatu zitawahakikishia Wananchi kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

Hata hivyo mara nyingi mechi dhidi ya Coastal Union sio nyepesi, timu hiyo imekuwa na kawaida ya kuipa changamoto Yanga katika mechi zake ingawa Yanga imekuwa na takwimu nzuri inapocheza dhidi ya Coastal katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwa ushindani uliopo kwenye ligi, Yanga haipaswi kudondosha alama katika uwanja wake wa nyumbani

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na kikosi chao kamili, hawana majeruhi zaidi ya mlinda lango Aboutwalib Mshery

Ni nafasi nyingine kwa mshambuliaji kinara wa mabao Fiston Mayele kuendelea kujiimarisha katika mbio za kuwania ufungaji bora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’