Yanga inakaribia kukamata 'mkwanja mrefu' ligi ya mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2018
Yanga inakaribia kukamata 'mkwanja mrefu' ligi ya mabingwa
Mchezo wa Yanga wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ni wa kufa na kupona kwa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo.

Yanga inahitaji kuiondosha Township Rollers kwenye michuano hiyo ili iweze kutinga hatua ya makundi na kujihakikishia kukamata kitita cha zaidi ya Bil 1.1.

Kama Yanga itafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa vilabu barani AFrika, kiasi cha pesa watakacholipwa ni karibu mara 12 ya pesa anayolipwa bingwa wa ligi kuu ya Vodacom!

Bingwa wa ligi kuu ya Vodacom analipwa Mil 80 wakati Yanga ikifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa itajihakikishia kukamata zaidi ya Bil 1 bila kujumuisha mapato ya uwanjani itakayopata katika michezo yake.

Viongozi wa Yanga wamejipanga kuhakikisha Yanga inapenya hatua hiyo msimu huu baada ya kosakosa ya msimu uliopita ambapo ilitolewa na Zanaco ya Zambia kwa faida ya bao la ugenini.

Habari njema zaidi ni kwamba hata kama Yanga itaondoshwa na Township Rollers, itahamia kwenye michuano ya kombe la shirikisho raundi ya pili ambayo kama watafuzu watatinga hatua ya makundi.

Lakini lengo namba moja la Yanga kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Hussein Nyika, ni kuhakikisha inafuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.

Kwa miaka kadhaa Yanga imekuwa ikipangwa na timu kutoka nchi za kiarabu hasa Misri katika hatua kama hii.

Lakini kwa misimu miwili sasa, Yanga inapata wapinzani wanaofungika, muhimu ni kujipanga vema.

Aidha kuwa na kocha kama George Lwandamina mwenye uzoefu wa michuano hii ni faida nyingine kubwa kwa Yanga.

Misimu miwili iliyopita, akiwa kocha wa ZESCO, Lwandamina aliwaongoza mabingwa hao wa Zambia kutinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kufanya vizuri kwenye hatua ya makundi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
52m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’