Wananchi wametoroka na alama zote tatu uwanja wa Benjamin Mkapa wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu
Feisal Salum 'Fei Toto' ameibuka shujaa kwa mara nyingine akifunga bao la ushindi dakika za majeruhi baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Farid Mussa
Prisons walitumia mbinu ya kupaki basi na kufanya mashambulizi kwa kushitukiza
Lakini haikuwasaidia kwani Feisal akawalaza na viatu dakika za jioni na kuirudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 35
Wananchi sasa wana uhakika wa kumaliza duru ya kwanza wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi
Wanaliaaaaaaaaaa...!




ADVERTISE HERE