Kauli ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Bodi ya Ligi Karim Boimanda kuwa Yanga kuvaa jezi toleo la tatu katika mechi mfululizo wanakiuka kanuni, ni mwendelezo wa yanayosemwa kuwa 'unbeaten' ya Yanga inawatesa wengi
Yani sasa Bodi ya Ligi ni kama inataka kuwapangia Yanga wavae jezi gani katika mechi zake wakati mavazi ya mchezo husika hupitishwa kwenye kikao kabla ya mechi (pre-match meeting)
Yanga ina maamuzi ya kutumia jezi gani katika kila mchezo ili mradi tu jezi hiyo imepitishwa kwenye kikao cha mechi
Iwe jezi toleo la kwanza, la pili au tatu, bado ni ya klabu ya Yanga, wenye maamuzi ya jezi ipi wavae ni Yanga wenyewe
Kwa hakika mateso ni makali, hata walio mafichoni wameanza kujitokeza......!
ADVERTISE HERE