Wakati Yanga ikiendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa ligi licha ya kucheza mechi pungufu dhidi ya wapinzani wake Azam na Simba, vita yao ya kuwania nafasi ya pili imepamba moto
Ikiwa imeshuka dimbani mara 12, Yanga inaongoza ligi na alama 32 sawa na Azam Fc ambao hata hivyo wamecheza mechi 14
Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na Azam Fc
Mchuano ni mkali katika nafasi ya pili Azam Fc wakionekana kupania kwelikweli kujimilikisha nafasi hiyo ili kuwashusha Simba katika nafasi ya tatu!
Yanga itajikita zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi kama itaibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc hapo kesho

ADVERTISE HERE