Fiston Mayele amewawashia taa nyekundu wapinzani wake katika mbio za kuwania ufungaji bora akifikisha mabao 10
Jana Mayele alifunga mabao yote ya Yanga katika mchezo dhidi ya Mbeya City uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Ni kasi ya aina yake ya kuzifumania nyavu kwa Mayele akifunga mabao saba katika mechi tatu
Mayele amedhamiria kuibuka na kiatu cha ufungaji bora msimu huu baada ya kukikosa msimu uliopita kwa tofauti ya bao moja dhidi ya George Mpole aliyefunga mabao 17
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Ihefu Fc na utapigwa Jumanne, Novemba 29 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya
ADVERTISE HERE