Matchday : Yanga vs Mbeya City, NBC PL, Nov 26

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2022
Matchday : Yanga vs Mbeya City, NBC PL, Nov 26

Jioni ya leo Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa kuanzia saa 12:15 jioni

Mechi nyingine ngumu kwa Wananchi kuwania alama tatu katika uwanja wa nyumbani

Ugumu wa mchezo huo unatokana na rekodi ya mechi za karibuni ambazo timu hizo zimekutana kwenye ligi

Katika mechi sita, Yanga iliibuka na ushindi katika mechi moja huku mechi tano zikimalizika kwa matokeo ya sare

Takwimu za msimu huu zinaibeba Yanga kuelekea mchezo huo ingawa Mbeya City nao ni timu ngumu kufungika

Kwa wastani Mbeya City ni timu iliyopata sare katika mechi zake nyingi msimu huu (7), ikishinda mechi nne na kupoteza mechi mbili

Yanga ina sare mbili tu na kushinda mechi nyingine (9) ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi

Leo kunako dimba la Mkapa kutakuwa na vita ya washambuliaji wawili wenye rekodi nzuri msimu huu Fiston Mayele na Sixtus Sabilo

Mayele anaongoza mbio za ufungaji bora akiwa na mabao 8 wakati Sabilo yuko nafasi ya pili akiwa amefunga mabao 7 lakini pia akiwa ametengeneza mabao 6

Kikosi cha Yanga leo kitaongezewa nguvu baadhi ya wachezaji waliokosa mechi zilizopita wakirejea

Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki, Benard Morrison, Farid Mussa na Yannick Bangala wote wako tayari kwa mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’