Ninja atolewa gozi gumu, aanza mazoezi mepesi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
21 Feb 2018
Ninja atolewa gozi gumu, aanza mazoezi mepesi
Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' ameanza mazoezi mepesi baada ya kutolewa plasta ngumu ‘P.O.P.’ katika mguu wake.

Ninja amesema baada ya kugundulika kuvunjika sehemu ya mfupa katika kifundo chake cha mguu wa kushoto aliwekewa plasta ngumu kuweza kuunga sehemu hiyo ambayo tayari imetolewa Februari 15 wiki iliyopita.

Beki huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea Taifa ya Jang'ombe ya Zanzibar alisema ameanza mazoezi mepesi kisiwani huko akianza kukimbia taratibu.

"Kwa sasa sihisi tena maumivu katika jeraha hilo ambapo nitaendelea kujifua taratibu kurudisha ubora wangu mpaka hapo daktari atakaponiruhusu kufanya mazoezi makali.

"Nashukuru Mungu Alhamisi iliyopita nilitoa ile P.O.P na baada ya kutoa niliambiwa nitembee taratibu na sikuwa nahisi tena yale maumivu kama awali,"amesema Ninja.

"Nimemaliza hatua ya kutembea na sasa nimeanza kukimbia taratibu ufukweni najisikia niko sawa,naamini nitarudi katika hali yangu ya awali niweze kuisaidia timu yangu."

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →