Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Liti, Singida
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Nabi alisema wamekuwa na muda wa kufanya maandalizi ya mchezo huo huku akipongeza ubora wa uwanja wa Liti
Nabi amesema amezunguka Tanzania na kucheza katika viwanja mbalimbali, ameridhishwa na ubora wa uwanja wa Liti licha ya kuwa haujawa sawa kwa asilimia 100
"Nawapongeza wamiliki wa uwanja wa Liti, haujawa bora kwa asilimia 100 lakini ni sehemu nzuri kwa kucheza mpira"
"Tusisubiri kusema viwanja vikiwa vibovu, hapa Singida wamejitahidi sana na wanastahili pongezi," alisema Nabi
Aidha Nabi alizungumzia mwenendo wa kikosi chake kucheza mechi nyingi mfululizo pasipo nkupoteza kwenye ligi akibainisha kuwa ni kazi wanayofanya kuwaandaa wachezaji kucheza kwa ajili ya kushinda bila ya kujali changamoto zinazowakabili na pia wafahamu ukivaa jezi ya Yanga inapaswa kupambana
"Tunawafundisha wachezaji kuwa na akili ya kushinda bila ya kujali changamoto yoyote ile. Tunawaambia ukivaa jezi ya Yanga inatakiwa kupambana kushinda mechi. Ni kitu kizuri watu wanahamasika na kushangilia Rekodi yetu ya kutokupoteza mchezo, inatupa morali ya kuzidi kupambana kushinda mechi nyingi zaidi"