Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said jana aliweka bayana kuwa wanatarajia kufanya maboresho ya kikosi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa ili kuhakikisha wanakuwa imara kuelekea mechi za makundi kombe la Shirikisho
Katika dirisha la usajili lililopita, Yanga iliongeza wachezaji sita wa kigeni Lazarus Kambole, Gael Bigirimana, Tuisila Kisinda, Stephane Aziz Ki, Joyce Lomalisa na Bernard Morrison
Kisinda alichukua nafasi ya Kambole ambaye hakucheza hata mechi moja ya mashindano baada ya kupata majeraha
Bigirimana na Kisinda ni kama bado hawajafikia matarajio ya Wananchi na pengine wanaweza kuwa kwenye presha kuelekea dirisha dogo
Mchezaji mwingine ambaye yuko katika presha kubwa juu ya hatma yake ni mshambuliaji Heritier Makambo ambayo bado anapambana kusaka makali yake
Katika dirisha dogo Yanga huenda itaongeza mlinzi wa kati wa Kimataifa ili kuimarisha safu ya ulinzi
Yannick Bangala anatumika nafasi ya ulinzi ili kukidhi mahitaji ya eneo hilo kwa sasa ingawa ni mahiri zaidi anapotumika kama kiungo mkabaji
Safu ya ushambuliaji pia inatarajiwa kuongezewa nguvu, Yacouba Songne nae amepona majeraha na anaweza kurejeshwa kikosini
Songne anafanya vizuri kwenye viwanja vya mazoezi Avic Town nafasi ya kurejeshwa kikosini ni kubwa
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ndiye atakayeamua maboresho ya timu yake ingawa ni wazi yatakuja na gharama kwani kuna wengine watapisha kwa kuuzwa au kwa makubaliano ya pande mbili