FT : Kagera Sugar 0-1 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2022
FT : Kagera Sugar 0-1 Yanga, NBC PL

Yanga imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo katika ligi kuu ya NBC wakiichapa Kagera Sugar bao 1-0 katika mchezo mgumu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Bao la Clement Mziza katika kipindi cha kwanza lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo akimalizia krosi ya Feisal Salum 'Fei Toto' kutoka upande wa kulia

Athari ya kucheza mechi mfululizo imeonekana katika mchezo huo kwani wachezaji walilazimika kufanya kazi ya ziada hasa kwenye kipindi cha pili kuweza kuondoka na alama tatu

Mlinda lango Djigui Diarra anastahili kuwa nyota wa mchezo huo akiokoa mkwaju wa penati pamoja na kuhakikisha haruhusu bao katika nyavu zake

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema walilazimika kufanya mabadiliko ya mbinu akitumia walinzi watano nyuma kutokana na uchovu pamoja na hali ya uwanja wa CCM Kirumba ambao ulijaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha muda mfupi kabla ya mchezo

Ni alama tatu ngumu zenye thamani kubwa ambazo zimeirudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’