Droo ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho itapigwa Jumatano, ijayo Novemba 16 jijini Cairo, Misri
Yanga ni miongoni mwa timu 16 zinazosubiri droo ya Shirikisho ikiangukia katika poti namba 2 sambamba na klabu ya DC Motema Pembe ya DR Congo
Timu zimepangwa kulingana na idadi ya pointi ambazo zimekusanya kwenye michuano ya CAF katika miaka mitano iliyopita
Yanga ina alama 0.5 zilizotokana na ushiriki wao katika hatua ya makundi ya Shirikisho mwaka 2018 na kumaliza kwenye nafasi ya nne
Poti namba 1 ina TP Mazembe, Pyramids, Asec Mimosas na USM Alger
Poti namba 2 ina timu za Motema Pembe na Yanga, timu nyingine zitaongezwa kupitia droo maalum kutoka katika timu 10 ambazo hazina alama. Droo hiyo pia itaunda poti namba 3 na 4
Kila kundi litakuwa na timu moja kutoka kila poti na timu zitazokuwa kwenye poti moja hazitakutana kwenye hatua ya makundi
