Jana baada ya mchezo dhidi ya Club Africain kumalizika na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huko Tunisia, kulitokea matukio ya vurugu ambapo baadhi ya wachezaji wa Club Africain na mashabiki wao walijaribu kuwashambulia wachezaji wa Yanga hasa Fiston Mayele
Lilikuwa tukio baya sana na hakuna shaka Shirikisho la Soka barani Afrika litachukua hatua
CAF imekuwa na msimamo mkali kwa matukio ya vurugu viwanjani
Lakini la kushangaza ni kuwa huoni tukio hilo likimulikwa na vyombo vya habari hapa nchini, ni kama hakuna jambo lililowatokea
Club Africain walipokuja kucheza na Yanga Dar kuna sintofahamu ilitokea katika chumba cha Wanahabari ikimuhusisha Meneja wa Digitali wa Yanga Privaldinho
Halikuwa tukio kubwa sana kwani Priva alikuwa akihoji uhakali wa Club Africain kutumia chumba cha wanahabari kubadilisha nguo wakati kipo chumba maalum kwa ajili yao
Kama tukio hili walilofanya Club Africain lingefanywa na Yanga dimba la Mkapa, mijadala ingefurika kila kona