Afya ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji bado haijaimarika vizuri baada ya kulazimika kufanyiwa upasuaji mwingine mdogo na kuwekewa chuma katika mshipa mmoja wa damu.
Kulingana na gazeti la Champion, mwezi uliopita, Manji alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kufanyiwa upasuaji huo mdogo.
Kutokana na upasuaji huo, Manji amewekewa vyuma viwili ndani ya mwaka mmoja tangu ashitakiwe kwa tuhuma ya matumizi ya dawa za kulevya. Alifanyia upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Kulingana na gazeti hilo, madaktari wameeleza si salama kwa Manji kufanyiwa upasuaji wa namna hiyo ndani ya mwaka mmoja.
“Angalau miaka minne au mitatu, lakini yeye ni mwaka mmoja amewekewa vyuma mara mbili. Daktari ameonya kwamba si jambo jema kiafya,†kilieleza chanzo.
“Hata hivyo, wamekuwa wakifanya siri sana. Unajua amekuwa na presha sana kutokana na matatizo yanayomuandama. Kuna wafanyakazi zaidi ya 4,750 waliokuwa wanafanya kwa Manji ilibidi waondolewe maana kampuni zake zote zimefungwa.
“Hii inaonekana kumchanganya sana, ndiyo maana amekuwa akiumwa na alikatazwa hata kuzungumza na simu hadi wiki moja iliyopita.â€
Juhudi za kumpata Manji zilifanyika na juzi jioni alipatikana, naye alipoulizwa akagoma kufafanua zaidi ya kuthibitisha kweli alilazwa.
“Ndiyo ninaumwa, nililazwa Aga Khan. Sasa mimi sipendi kuzungumza mambo yangu ya ugonjwa kwenye vyombo vya habari,†alisema.

ADVERTISE HERE