Nabi amejipanga kuwaadhibu Club Africain kwao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
7 Nov 2022
Nabi amejipanga kuwaadhibu Club Africain kwao

Wachezaji wa Yanga watakuwa dakika 90 muhimu za kupambana katika mchezo wa mkondo wa pili kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ya Tunisia

Yanga iko nchini Tunisia ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo wakiweka kambi nje kidogo ya mji, Sousse

Akizungumza juzi baada ya kutua Tunisia, kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alisema anatarajia mchezo huo ambao utapigwa Jumatano, Novemba 09 utakuwa tofauti na mchezo waliocheza jijini Dar es salaam wiki iliyopita

Katika mechi hiyo, Yanga inahitaji sare yoyote ya mabao ama ushindi ili kufuzu na kama matokeo yatakuwa suluhu, basi changamoto ya mikwaju ya penati itaamua mshindi

Nabi alisema anafahamu ubora wa Club Africain wanapocheza nyumbani hivyo amewaelekeza wachezaji wake kuwa makini ili kuhakikisha hawafungi bao mapema

"Hatutaki kuruhusu wapate bao mapema, mabeki wetu wanapaswa kuwa makini zaidi na washambuliaji wao, tunafahamu mechi yao ya mwisho nyumbani walishinda mabao 7-0 dhidi ya Kipanga.

"Katika mechi hiyo walifunguka kwa sababu wako nyumbani, ugenini hawakucheza hivyo, kwa kuwa tumeona ubora wao hatutakiwi kuwapa nafasi," alisema Nabi

Nabi alisisitiza mchezo wa siku ya Jumatano utakuwa tofauti na wamejipanga  kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri katika mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →