Matchday : Geita Gold vs Yanga, NBC PL Oct 29

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2022
Matchday : Geita Gold vs Yanga, NBC PL Oct 29

Wananchi wako jijini Mwanza ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kusaka alama zote tatu ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi

Hata hivyo ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na ubora wa timu zote

Kuna aina ya ushindani umejengeka kati ya Geita Gold na Yanga hasa kwa kuangalia matokeo ya msimu uliopita licha ya Yanga kushinda mechi zote tatu katika mashindano yote

Kwa mara ya kwanza Saido Ntibazonkiza aliyeitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa msimu uliopita, leo anakutana na waajiri wake hao wa zamani

Saido anaweza kuwa mchezaji na kutizamwa zaidi kwa upande wa Geita Gold kwani anaifahamu vyema Yanga na leo atatamani kuwaadhibu waajiri wake hao wa zamani

Yanga ilitua Mwanza mapema jana na jioni ikafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi atautumia mchezo dhidi ya Geita Gold leo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Jumatano, Novemba 02

Leo Nabi anaweza kuwarejesha kikosini Fiston Mayele, Kibwana Shomari na Djuma Shabani ambao walikosa mchezo uliopita dhidi ya KMC

Djuma na Mayele walikuwa na majeraha madogo lakini jana walishiriki mazoezi ya mwisho kikamilifu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’