Kama kuna mtu anadhani kucheza mechi 44 pasipo kupoteza kwenye ligi ni kitu rahisi basi waulize Simba
Simba leo wametepeta mbele ya Azam Fc wakichapwa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube
Hawa Azam Fc wako vizuri msimu huu licha ya matokeo mabaya waliyopata katika mechi kadhaa kwenye ligi na kombe la Shirikisho
Azam Fc pia walifanikiwa kupata alama moja dhidi ya Yanga katika mchezo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Yanga sasa imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 17, wakifuatiwa na Mtibwa Sugar wenye alama 15
Simba iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 14. mapemaaaa Wananchi wanauanza mwendo wa ubingwa wa 29

ADVERTISE HERE