Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa klabu ya Yanga, Hussein Nyika alikwenda nje ya nchi kufuatilia baadhi ya wachezaji ambao wanataka kusajiliwa.
Aliahidi wikiendi hii angeweza kuweka hadharani majina ya wachezaji wengine wapya ambao wamesajiliwa huku mwenyewe akiita 'kuachia bomu la kunyikilia' kutokana na hadhi za wachezaji hao.
Hilo halikufanyika wikiendi hii ni kwa sababu bado kiongozi hajamaliza kuweka mambo sawa kwa baadhi ya wachezaji.
Katibu Mkuu Charles Mkwasa 'Master' amesema, ni Mwenyekiti wa Kamati ya usajili anayesubiriwa akamilishe kazi yake ili kila kitu kiwe hadharani.
Mwaka huu uongozi umeamua kufanya usajili wa 'kimyakimya' ambao nadhani umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwapata wachezaji waliohitajika.
Ni wachezaji wawili tu waliokosekana ambao klabu iliwahitaji.
Nadhani WanaYanga tuendelee kuwa na subira. Ngoja viongozi wamalize jukumu hilo halafu wataanika kikosi hadharani.
Tusichanganywe na habari za kwenye magazeti na 'vijiweni' kwani wengine wanafanya hivyo kuuza magazeti yao si unajua Yanga timu kubwa!
Kwa vyovyote zoezi la usajili litakamilika mapema kwa kuwa kocha Lwandamina ameagiza usajili ukamilike haraka ili wachezaji wapya wapate muda wa kuzoeana.

ADVERTISE HERE