Matchday : Yanga vs Simba, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2022
Matchday : Yanga vs Simba, NBC PL

Baada ya tambo za hapa na pale kwa takribani wiki nzima, hatimaye ile siku ya HUKUMU imewadia

Ni mtanange wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni

Mchezo wa ligi kuu ya NBC, matokeo ya mchezo huo yataamua nani anaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi timu zote zikiwa na alama 13 Simba ikiwa juu ya msimamo kwa tofauti ya mabao tu

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga ili kurejesha furaha ya mashabiki wake baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Takwimu zimeendelea kuibeba Yanga ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya watani zake katika michezo ya karibu ambapo katika michezo mitano iliyopita Yanga imeshinda mitatu na kutoka sare michezo miwili

Hata hivyo katika mechi za dabi, takwimu pekee hazitoshi kuihakikishia timu ushindi bali zinaweza kuwa chachu kwa timu kupambana ili kupata matokeo

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na uhakika wa kumkosa mchezaji mmoja Bernard Morrison anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu

Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' naye yuko kwenye hatihati akiwa amerejea mazoezini siku chache zilizopita akitoka kuugua malaria

Ari na morali ya wachezaji wa Yanga iko juu kuelekea mchezo huo wakiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi

Kila la kheri Wananchi....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’