Yanga yasaini mkataba na Umoja wa Mataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2022
Yanga yasaini mkataba na Umoja wa Mataifa

Klabu ya Yanga leo imeingia mkataba wa Ushirikiano na UNICEF ambalo ni Shirika la Umoja wa Taifa (UN) kwa ajili kutoa elimu ya maradhi ya Covid 19 na Ebola

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mkataba huo wa miezi sita ni matunda ya Ushirikiano kati ya Yanga na Kampuni ya Jackson Group iliyofanikisha mkataba huo kusainiwa

"Sisi kama klabu ya Wananchi tumekuwa tukifanya matukio mbalimbali yanayokwenda kugusa jamii moja kwa moja katika mechi zetu. Yanga imetengeneza mfumo ambao unairudisha kwenye jamii kupitia ushirikiano na kampuni ya GSM Foundation"

"Mahusiano haya yameivutia sana UNICEF na Umoja wa Mataifa kwaa ujumla na kuona kama klabu hii inaweza kuwa na athari kati kufanikisha miradi ambayo inakwenda moja kwa moja kwenye jamii"

"Kupitia hapo Yanga imepewa nafasi ya kuwa Mshiriki wa UNICEF katika miradi mikubwa ambayo inagusa Jamii moja kwa moja. Mkataba tuliosaini unakwenda kuingunisha Yanga na UNICEF kupitia miradi mikubwa miwili"

"Mradi wa kwanza ni chanjo ya UVIKO 19 ambalo sote tunafahamu ni janga la dunia. UNICEF imeona klabu ya Yanga inaweza kufanikisha mradi huu kwa Watanzania"

"UNICEF wametupa jukumu la kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO-19"

"Yanga pia inakwenda kufanya kazi na UNICEF kutoa elimu wa Watanzania kuhusu janga la Ebola ambalo sote tumesikia nchi ya Uganda imetangaza kuna ugonjwa wa Ebola ambao umeshaanza kuingia katika nchi hiyo "

"Miradi hii inakwenda kuigusa jamii moja kwa moja na UNICEF wameona klabu ya Yanga inaweza kushirikiana nao katika kutoa elimu ya majanga haya"

Hersi amesema Yanga imechaguliwa na UN baada ya kukidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kukaguliwa hesabu za klabu na mfumo wa Uendeshaji wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’