Majira ya saa tatu usiku leo, Yanga itakuwa dimbani kule Sudan kumenyana na Al Hilal
Ni mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika, kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na mahitaji ya ushindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam wiki iliyopita
Kwa hakika ni mchezo muhimu sana kwa Yanga, wakihitaji ushindi ili kutinga hatua ya makundi
Yanga ilitua Sudan jana majira ya mchana na usiku vijana wa kocha Nasreddine Nabi wakapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Al Hilal utakaotumika leo
Hautakuwa mchezo mwepesi lakini ni wazi Yanga imekwenda Sudan ikiwa na lengo moja tu, kupata ushindi
Wananchi tutaheshimu matokeo ya mchezo baada ya dakika 90 lakini matumaini ni makubwa siku ya Jumatatu itakuwa maalum kwenda kuipokea timu pale uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa nchi...