Tuendelee kumsubiri Kamusoko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2018
Tuendelee kumsubiri Kamusoko
Kumekuwa na sintofahamu juu ya kiungo Thabani Kamusoko ambaye uongozi wa Yanga umesema tayari amepona majeraha yake lakini bado haonekani dimbani.

Wengi walitarajia mchezo wa jana dhidi ya Majimaji angeweza kuwa sehemu ya kikosi lakini alikosekana hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba

Shauku ya mashabiki kumuona Kamusoko uwanjani inadhihirisha ni kiasi gani anavyokubalika.

Tangu ajiunge na Yanga misimu miwili iliyopita, Kamusoko ameifanyia Yanga mambo makubwa na ndio maana wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kumuona akirejea kikosini

Wengi wanaamini uwepo wake dimbani utaongeza kitu sehemu ya kiungo ya Yanga ambayo kwa sasa inamtegemea zaidi Tshishimbi.

Hata hivyo benchi la ufundi ndilo linalofahamu zaidi juu ya hali za wachezaji hivyo lazima maamuzi yao yawe ya mwisho.

Kamusoko amekaa nje kwa muda mrefu (tangu Septemba 2017) kurejea kwake uwanjani kunafaa kuwe kwa tahadhari kubwa.

Hatari ya mchezaji kurejea kiwanjani haraka ikiwa bado hayuko fiti itapelekea majeraha zaidi

Pengine hicho ndicho kilichomkumba Amissi Tambwe ambaye mashabiki walikuwa na shauku kubwa ya kumuona akirejea lakini sasa tayari amerudi kwenye orodha ya majeruhi.

Hapa jambo la msingi ni kuliacha benchi la ufundi lifanye kazi yake, kwa kuwa wao ndio wanajua hali za kila siku za wachezaji.

Sisi mashabiki tunaweza kuwa na wachezaji tunaowapenda sana lakini kama kocha anaona hawako tayari kimchezo basi tuvumilie.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’