Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kimerejea Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Mchezo huo utapigwa Sudan, Jumapili Oktoba 16 katika uwanja wa Al Hilal, saa mbili usiku kwa saa za Tanzania
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewahakikishia Wananchi kuwa bado nafasi ya kutinga hatua ya makundi wanayo kwani wanajipanga kwenda kupata ushindi hukohuko ugenini
Nabi aliyewahi kuifundisha Al Hilal, amesema ana uzoefu na soka la Sudan hivyo anafahamu ni aina gani ya maandalizi wanahitaji ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
Yanga itahitaji ushindi wa aina yoyote Sudan au matokeo ya sare kuanzia mabao mawili ili kutinga makundi
ADVERTISE HERE