Tuko tayari kuikabili Al Hilal - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2022
Tuko tayari kuikabili Al Hilal - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wako tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Nabi amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo katika mpango wao wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi

Amesema wanakwenda kuchuana na Al Hilal ambao pia wana mahitaji kama yao hivyo utakuwa mchezo wenye upinzani mkali

"Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu unaotarajiwa kuwa mgumu. Wachezaji wako tayari, wanajiamini lakini pia wakiwaheshimu wapinzani wetu Al Hilal"

"Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu ni mashindano makubwa na ifahamike mshindi wa kwenda hatua inayofuata ataamuliwa baada ya mchezo wa pili kule Sudan"

"Wachezaji wanafahamu hilo, wana uzoefu wa michuano ya aina hii wanajua vile wanapaswa kucheza ili kuweza kupata matokeo mazuri nyumbani," alisema Nabi

Nae kiungo Gael Bigirimana amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingo katika mchezo huo kuwapa hamasa wachezaji

Gael amesema itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika lakini wachezaji wengi wa Yanga wana uzoefu wa kushiriki michuano hiyo

Amesema wachezaji wote tayari na dhamira yao ni kupata ushindi ili kuwa na nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’