Mshambuliaji Obrey Chirwa amefunga moja ya mabao ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18 ambapo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Baada ya kupachika bao hilo kwenye dakika ya 29, Chirwa alivua jezi yake kuonyesha ujumbe aliouandika katika fulana yake ya ndani unaosomeka kwa lugha ya kingereza 'NEVER GIVE UP' kwa maana hakuna kukata tamaa.

Hilo lilikuwa bao lake la 11 msimu huu akizidi kumkaribia Emanuel Okwi wa Simba anayeongoza orodha ya vinara wa mabao akiwa na mabao 13.
Chirwa pia alisababisha mkwaju wa penalti kwenye dakika ya 19 baada ya shuti lake lililokuwa linaelekea kimiani kuokolewa kwa mkono na beki wa Majimaji.
Pengine baada ya lawama nyingi, Chirwa leo hakuchukua jukuma la kupiga penalti hiyo ambapo alimuachia kiungo Papi Tshishimbi aliyefunga kwa ustadi mkubwa.
Chirwa amedhihirisha Uungwana wake, aidha kujituma kwake dimbani kunamfanya awe silaha muhimu sana ya Yanga kwa sasa.

ADVERTISE HERE