Aliyekuwa Msemaji/Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha hakuna nafasi inabaki kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Manara ambaye anaendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili, amesema mashabiki wa Yanga watafanya makosa makubwa kama watadhani ubora wa kikosi chao pekee utatosha kuwapa ushindi dhidi ya Al Hilal pale uwanja wa Mkapa
"Niwahakikishie ushindi wetu wa Jumamosi hauwahitaji wachezaji pekee, tunajhitaji sote kila mmoja kwa nafasi yake ajitoe Kwa ajili ya Club hii, ndio tutapata tukitacho"
"Lazima Washabiki wawe full house, narudia ni full house uwanjani,ili kuwapa nguvu Wachezaji wetu. Na hapa nguvu yenyewe ni kushangilia mwanzo mwisho na kuzomea wapinzani wetu kila wakigusa mpira. Kama kuna mechi tunawahitajia mashabiki zaidi ni mechi hii ya Jumamosi dhidi ya Al Hilal. Nunua sasa Tiketi yako uje kusapoti Wananchi," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia vituo vilivyoainishwa pamoja na mitandao ya simu