Jana mshambuliaji Fiston Mayele alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga waliupata dhidi ya Mbuni Fc katika mchezo wa ndani wa kirafiki uliopigwa Avic Town
Mayele pia alifunga mabao mawili katika mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Eagle Fc ambao ulipigwa siku chache zilizopita hapohapo Avic Town na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
Ikumbukwe Mayele alitoka kufunga mfululizo katika michezo dhidi ya Zalan Fc (3), Mtibwa Sugar (1) na Zalan Fc (3) na kumfanya awe amefunga mabao 10 katika michezo mitano iliyopita
Mchezo pekee ambao hajatetema msimu huu ni dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Kwa hakika msimu huu unaweza kuwa bora sana kwa Mayele ambaye kiu yake ya kuzifumania nyavu haikauki
Mayele hachagui wa kufunga, wadogo na wakubwa wote amewatetemesha