Tuna kikosi bora kuliko Al Hilal - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2022
Tuna kikosi bora kuliko Al Hilal - Kamwe

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amewahakikishia wapenzi na wanachama wa timu hiyo kuwa wana nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa kwa kupata ushindi dhidi ya Al Hilal kutokana na ubora wa kikosi chao

Katika mahojiano na Wasafi Fm, Kamwe amesema Wananchi hawapaswi kutishwa na wachambuzi ambao wanatumia historia ya Al Hilal ya miaka ya nyuma pasipo kuangalia ubora wa timu zote kwa wakati huu

"Sisi tunawaheshimu Al Hilal kwa historia yao lakini nasema kwa wakati huu tuna timu nzuri kuliko wao. Ukiangalia bado wanahangaika kujenga timu yao lakini sisi tumeshalifanya zoezi hilo misimu minne iliyopita"

"Tumecheza mechi 41 mfululizo ligi kuu pasipo kupoteza mchezo, kama wangekuwa Al Hilal ndio wana rekodi hii basi pengine vitisho kwa Yanga ingekuwa zaidi"

"Tunajua jambo pekee wanalojivunia ni vurugu za mashabiki wao nje ya uwanja, sasa sisi tumejipanga tutawaonyesha kuwa tuna wazimu wa soka kuliko wao. Kesho tutazungumza na wanahabari kuweka mkakati wa mchezo huo. Mechi itachezwa saa kumi lakini tutahakikisha mpaka saa sita mchana uwanja umejaa na tutacheza na kuimba tukiwasubiri uwanjani," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’