Andrey Mtine Mtendaji Mkuu wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2022
Andrey Mtine Mtendaji Mkuu wa Yanga

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Mzambia Andrey Mtine kuwa Mtendaji Mkuu wa Yanga (CEO)

Akizungumza katika utambulisho wa bosi huyo mpya wa Yanga, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema Mtine amesaini mkataba wa miaka miwili

Hersi amesema wamemuajiri Mtine kutokana na uzoefu wake katika uongozi na usimamizi wa soka barani Afrika

Mtine amewahi kuhudumu kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa soka katika klabu za Nkana, Zesco United kule Zambia, CAF kama commisioner na TP Mazembe ambapo amefanya kazi katika klabu hiyo kwa miaka 12

Mtine amesema amejiunga na Yanga kutokana na historia ya klabu hiyo na anaamini ni nafasi kwake kutoa mchango wake katika kuhakikisha Yanga inafikia malengo yake

Katika hatua nyingine Yanga imetangaza kusajili Wanachama zaidi 40,000 huku ikizindua utaratibu wa kujisajili kidigitali kupitia website na App rasmi ya klabu ya Yanga

Kupitia Website na App, utaweza kujisajili kuwa Mwanachama na shabiki wa klabu ya Yanga na hivyo kuondoa ulazima wa kwenda kujisajili kwenye matawi

Kama huna 'Smart Phone' unaweza kujisajili kuwa Mwanachama au shabiki kupitia USSD

Kuhusu kadi, Injinia Hersi amesema changamoto ya ucheleweshwaji wa kadi imepatiwa ufumbuzi ambapo klabu imeleta printer za kisasa kutoka nje ya nchi ambazo zitaharakisha kuchapisha kadi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
25m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’