Ukikiangalia kikosi cha Yanga, utakubali kama kitashindwa kuvuka kwenda makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu basi viongozi watakuwa na wakati mgumu kujibu maswali nini wafanye ili kufanikisha hilo
Yanga ilianza kujipanga kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita, sasa Wananchi wako katika wakati wao bora sana
Sawa, Yanga haijacheza makundi ya ligi ya mabingwa kwa takribani miaka 24 lakini katika kikosi wana wachezaji ambao wamecheza michuano hiyo katika miaka ya karibuni
Joyce Lomalisa, Djuma Shabani, Yannick Bangala, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Bernard Morrison, Stephane Aziz Ki na Tuisila Kisinda hawa wana uzoefu mkubwa katika michuano hiyo
Katika ile AS Vita iliyokuwa ya 'moto' kwelikweli kina Djuma, Lomalisa, Kisinda, Moloko, Mayele na Bangala walikuwepo. Ni msimu uliopita tu, Kisinda alishinda kombe la Shirikisho akiwa na RS Berkane
Hawa akina Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Djigui Diarra, Feisal Salum, Farid Mussa, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Sure Boy ni wachezaji ambao wanao uzoefu wa kushiriki michuano mikubwa pia
Yanga inahitaji kupata ushindi dhidi ya Al Hilal ili kuweza kufuzu hatua ya makundi. Habari njema ni kuwa wachezaji sita katika kikosi chao wamewahi kufundishwa na Florent Ibenge, mkufunzi wa Al Hilal
Pengine Al Hilal ndio wanapaswa kuwa na hofu zaidi ya kukutana na Yanga hasa Ibenge ambaye anafahamu aina ya watu anaokwenda kukutana nao
Ni watu wanaozifahamu mbinu zake nje/ndani na watataka kudhihirisha ubora wao mbele yake
Oktoba 08 itakuwa siku ya kihistoria kwa Yanga na kwa hakika Wananchi wana kila sababu ya kushinda mchezo dhidi ya Al Hilal