Yanga yaiandalia kipigo Majimaji FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2018
Yanga yaiandalia kipigo Majimaji FC
Kikosi cha Yanga kimeweka kambi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Majimaji FC.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Jumatano, Februari 14 kwenye uwanja wa Taifa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Yanga kutumia uwanja huo kama mwenyeji katika michezo ya ligi tangu ufunguliwe baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja tu, kuhakikisha inaibuka na ushindi ili kuendelea kuwapa wakati mgumu vinara wa ligi, Simba.

Iwapo Yanga itakosa ushindi kwenye mchezo huo, itaipa Simba nafasi ya kuukaribia ubingwa kwani itahitaji kuhakikisha inashinda mchezo wake dhidi ya Mwadui FC keshokutwa.

Bahati mbaya msimu huu, michezo mingi ratiba imekuwa ikiitanguliza Yanga kucheza kabla ya Simba. Hivyo wapinzani wao wanakuwa na nafasi ya kufahamu matokeo yao kabla!

Hata hivyo Yanga imeshinda michezo karibu yote ambayo imetangulizwa. Hivyo bila shaka kesho itaendelea na mwendo huo huo.

Bado kuna michezo 13 ya kupigania kutetea ubingwa. Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema watahakikisha wanashinda michezo mingi wawezavyo ili hatimaye watetee ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.

Yanga imekuwa na rekodi nzuri kwenye duru ya pili ya ligi kuu ya Vodacom. Msimu uliopita ilitwaa ubingwa baada ya kushinda michezo yake mingi ya mzunguuko wa pili.

Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali msimu huu, Yanga bado inao uwezo wa kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’